Tuesday, December 23, 2008

SODOMA NA GOMORA PANAVYOONEKANA SASA

Ndugu wanaharakati wenzangu,nilipokuwa Israel nilifanikiwa kutembelea maeneo mengi ya ukombozi wa mwanadamu hasa ya kihistoria katika biblia.Nilipata kupaona Sodoma na Gomora ambako Mungu alipateketeza kwa moto.Mpaka sasa bado panatisha jamani.Hakuna mmea unaomea sehemu hizo na hakuna watu wanoishi.Kama picha inavyoonesha(bad terrain),ndivyo kulivyo.Hii inatufundisha nini?inatufundisha kuwa tuziache njia zetu mbaya,tumfuate Mungu anasema nini ili yasije kutupata kama ya Sodoma na Gomora.Utajiuliza,kama hili lilitokea hapa duniani je,huko mbinguni si ndio itakuwa balaa!!!
Tuziache dhambi.tutubu na kumrudia Mungu.Tuzishike amri na maagizo anayotuagiza kufanya.Mungu wetu ni mwema atatusamehe na kutusikiliza(Isaya 41:10) Picha: Sodoma na Gomora

No comments:

Followers