Tuesday, May 12, 2009

RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU YA 2008: TANZANIA

OFISI YA DEMOKRASIA, HAKI ZA BINADAMU NA KAZI

Ripoti za Nchi za mwaka 2008 kuhusu Mwenendo wa Haki za Binadamu

25 Februari, 2009

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yenye idadi ya watu takriban milioni 40, ni jamhuri inayofuata mfumo wa vyama vingi inayojumuisha bara na mkusanyiko wa visiwa vya Zanzibar; ambayo visiwa vyake vikuu ni Unguja na Pemba. Muungano unaongozwa na Rais ambaye pia ni mkuu wa serikali; chombo chake kimoja cha kutunga sheria ni Bunge la Taifa (Bunge). Pamoja na kwamba Zanzibar imeunganishwa kwenye mfumo wa serikali na chama wa nchi, ina Rais wake, mfumo wa mahakama na baraza la kutunga sheria na inaendelea kufanya mambo yake kwa uhuru. Kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 wa Rais na wabunge, Jakaya Kikwete alichaguliwa kuwa Rais, na chama tawala cha Mapinduzi (CCM) kilipata viti vingi bungeni. Waandalizi waliuona uchaguzi wa Muungano katika pande zote mbili za bara na Zanzibar kuwa ulikuwa huru na wa haki kabisa. Hata hivyo, uchaguzi wa 2005 wa Rais kwa upande wa Zanzibar ulikuwa na ubishani, wenye dosari kubwa na vurugu zilizochochewa kisiasa. Wakati viongozi wa kiraia kwa ujumla walidhibiti majeshi ya usalama, kulikuwa na matukio kadhaa ambapo askari wa majeshi ya usalama walifanya kazi peke yao bila ya uongozi wa serikali.
Kulikuwa na matukio kadhaa ya matatizo ya haki za binadamu yaliyokuwa yakiendelea. Polisi na walinzi wa magereza walitumia nguvu kubwa dhidi ya wafungwa au watuhumiwa, na wakati mwingine kufikia kusababisha vifo, na suala la polisi kutochukuliwa hatua limebaki kuwa ni tatizo; mazingira ya magereza yalikuwa mabaya na ya kutishia maisha; rushwa ilienea kwa kiasi kikubwa miongoni mwa polisi, na uvunjaji wa taratibu za kisheria; idara ya mahakama ilikabiliwa na rushwa na kukosa ufanisi hususan katika mahakama za mwanzo; uhuru wa kuzungumza na uhuru wa vyombo vya habari ulikuwa mdogo; tatizo la rushwa liliendelea kuwepo serikalini; mamlaka ziliwazuia wakimbizi kutembea; utumiaji nguvu dhidi ya wanawake katika jamii ulizidi; na biashara ya watu na ajira ya watoto yalikuwa ni matatizo.

Kwa habari zaidi tembelea http://tanzania.usembassy.gov/uploads/nt/d4/ntd46z8s_-4TmOq6VoxlTQ/ripoti_haki_za_binadamu_2008.pdf

No comments:

Followers