Friday, December 12, 2008

WATANZANIA: UKOMBOZI WA KIFIKRA NI HUU

Wapendwa,
Tumetawaliwa na wakoloni kwa kipindi kirefu.Kulikuwa na sauti zisizosikika.kulikuwa na vilio visivyoisha.Sasa tuko huru.uhuru wa mwaka 1961 hautoshi.uhuru wa kimawazo,kifikra,kiitikadi,kiuchumi na kijamii ndio uhuru halisi.Kwa nini bado tuna upeo mdogo?fikra zikiwa pana,kutakuwa na maendeleo,si tu ya mtu binafsi,bali ya nchi nzima.tuamke watanzania.Nchi imeliwa,inachukuliwa.tuwe na fikra maendeleo,si fikra mgando.Tusiwe wa kuamka na kusema tutafanyiwa nini na nchi hii yaani kuiba,bali tuwe wa kuamka na kusema tutaifanyia nini nchi kwa maendeleo ya wote.Isiwe UFISADI!
Mimi,
mwanenu,
magessa,b.m.

2 comments:

magessa,bm. said...

Kulikuwa na mjadala wa miaka 47 ya uhuru wa Tanzania hapo jana kwenye kipindi cha `KIPIMA JOTO'ITV-Tanzania.Wewe ungepata muda wa kupiga simu studio ungechangia nini?nini kimefanyika toka 1961 mpaka sasa 2008?je nchi bado ina dira?
mwanaharakati anakusikiliza

magessa,bm. said...

Uchaguzi wa TFF umekwisha na kwa mara nyingine tena Leodgar Tenga amechaguliwa kuwa Rais wake.Unadhani ni nini afanye zaidi ya alivyofanya kukiboresha chama?

Followers